Faida za Zinc
Zinc inahitajika katika kutengeneza vimeng’enya zaidi ya 100 mwilini na 75 kati ya hizi ni muhimu sana katika usagaji ya chakula mwilini(digestion).
👉🏾Ni muhimu sana katika utungisho (fertilization). Mbegu ya kiume kuweza kuliingilia yai la kike.
👉🏾Inasaidia mchakato wa kukua( growth)kwa mtoto. Mtoto anayepungukiwa zinc ana hatari ya kudumaa.
👉🏾Inazuia kumea kwa chunusi kwa kuwianisha mafuta katika ngozi.
👉🏾Inalinda na kuboresha afya ya korodani (protaste).
👉🏾Zinc inafanya vindonda vipone haraka.
👉🏾Inazuia kudhoofika kwa misuli kwa watu wenye umri mkubwa.
Inasaidia kinga dhidi ya upofu kwa watu wenye umri.
👉🏾Inaongeza uwezo kionjo(taste)na wa mnuso (smell).
👉🏾 Inadhibiti maradhi ya vileo ndani ya mwili.
👉🏾Inahusika na utengenezaji wa collagen. Hii protein inayoshikilia sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo mifupa.
👉🏾Inahusika na matumizi ya mwili (metabolism) ya vyakula vya wanga( carbohydrates).
👉🏾Inahusika na matumizi mwilini ya vitamin mbalimbali na hasa zile za aina ya B.